Wananchi wa kijiji cha Dongo kilichopo kata ya Kilindoni wanatarajia kuwa na Kituo cha Afya baada ya miaka mingi ya kukosekana kwa kituo cha kutolea huduma za afya kijijini hapo.
Hilo limewekwa wazi leo Mei 23, 2025 wakati wa kikao cha kutambulisha mradi huo ambapo Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Maulid Majala, akiambatana na baadhi ya wataalam wa Halmashauri, alifanya kikao hicho na halmashauri ya kijiji cha Dongo.
Jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni 250 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia ambapo fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza itakayohusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), vyoo pamoja na kichomea taka.
Dkt. Majala ametumia fursa ya kikao hicho kuwasisitiza viongozi wa kijiji kutoa hamasa katika jamii ili wananchi waweze kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa mradi huo pindi utakavyoanza ili wananchi wanufaike kwa wakati.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.