Kamati ya Lishe imefanya kikao cha kupitia mpango na bajeti ya Lishe kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Katika kikao hiki mgeni rasmi alikua Katibu Tawala (W) Bw. Gilbert Sandagila. Aidha alikuwepo mjumbe mmoja kutoka OR-TAMISEMI Bi. Asiatu Mbwambo na mjumbe mmoja kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Pamela Meena.
Afisa Lishe (W) aliwasilisha taarifa ya tathmini kwa kwa kuwapitisha wajumbe katika kazi zilizofanyika kwa mwaka wa 2022/2023 ikionesha hali ya lishe.
Taarifa ilibainisha asilimia za mafanikio kwamba;
Utoaji wa Vitamini 82.1%, shule zinazalisha chakula lishe 94.4%, Vijiji vinavyofanya shughuli za lishe 97.5%.
Pamoja na mafanikio hayo, kuna watoto waliogundulika kuwa na utapiamlo na kupewa dawa sawa na 60.6%. Wajawazito waliomeza dawa kuongeza damu (FEFO) ni 55.3, hali ya unyonyeshaji watoto chini ya miezi 6 ni 99%, Hali ya ukondefu kwa watoto kuanzia miezi 0 - 59 ni 08% shule zenye club ya shughuli za afya na lishe ni 69.4%.
Changamoto za lishe zinazoikabili Wilaya ni pamoja na lishe duni, uzito uliokithiri na upungufu wa vitamini na madini.
Mikakati iliyopo ni pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya lishe kwa jamii na matumizi bora na sahihi ya choo, kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimi juu ya lishe na kuweka mazingira wezeshi ili kuboreaha lishe, kuhamasisha kila shule waanzishe miradi ya ufugaji kuku na kilimo cha mbogamboga ili wanafunzi wapate lishe bora.
Wajumbe walishauri pia ianzishwe siku ya lishe kijijini ili kuhamasisha uboreshaji wa lishe.
Pia wajumbe wa kamati ya lishe (taasisi za dini, taasisi zisizo za kiserikali na idara zinazohusiana kama kilimo, mifugo, maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii, ) wawe wanawasilisha taarifa za lishe za maeneo yao.
Mjumbe kutoka utawi wa jamii alisema katika idara ya Maendeleo ya Jamii kuna kitengo kinachohusika na lishe kwa watoto yenye bajeti ya Tshs. 32m. Mjumbe kutoka RUWASA alisema kupitia mradi wa SWASH wana bajeji Tshs. 22 m. kwa ajili maji na maswala ya lishe.
Aidha Kitengo cha lishe kilipokea pikipiki tatu kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya shughuli za lishe.
KAZI IENDELEE
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.