Idara ya Elimu Sekondari iliandaa kikao kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kwa ajili kuwashukuru na kutoa taarifa ya mandeleo ya Elimu Sekondari.
Mgeni rasmi wa kikao hicho alikuwa Mh.Shaib Nnunduma Mkuu wa Wilaya ya Mafia aliyewakilishwa na Katibu tawala wake Ndugu Gilbert Sandagila ambaye alitoa hotuba fupi ya ufunguzi
Baada ya ufunguzi ilisomwa taarifa rasmi ya uendeshaji wa kambi kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2020 zilizowekwa katika shule mbili za sekondari 1. Bweni sekondari ambapo waliwekwa wanafunzi waliokuwa wanasoma masomo ya sanaa na 2. Kitomondo Sekondari ambapo waliwekwa wanafunzi waliokuwa wanasoma wa sayansi .
Kambi hizo mbili zilisimamiwa na kamati iliyoundwa na walimu chini ya ofisi ya Afisa Elimu Sekondari ambapo ilisaidiana na ofisi ya afisa Elimu Sekondari kuendesha na kusimamia shughuli zote za kambi
Kambi ilikuwa miezi mitatu kuanzia mwezi Julai 2020 hadi mwezi Novemba .2020, gharama za kambi hizo ni Tshs. 119,047,000 zikiwemo gharama za chakula Tshs. 75,332,000/=, shajala Tshs. 23,315,000/= na usafiri Tshs. 20,400,000/=
Pia waliwashukuru wahisani mbali mbali waliojitokeza hata kufanikisha zoezi zima la kambi wakiwemo:-
Katika kikao hicho pia iliwasilishwa taarifa ya matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ambapo wanafunzi waliofanya mtihani kwa mwaka 2020 ni 437 na walifaulu kwa 88.9% na mwanafunzi waliopata daraja 0 (Division zero) ni 48 tu ukilinganisha na mwaka 2019 waliofanya mtihani wanafunzi 427 na ufaulu ulikuwa 67% waliopata daraja sifuri (Division 0 ) walikuwa 140
Changamoto mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliana namna ya kuzitatua pia michango mbalimbali ya namna ya kuanzisha na kuendesha tena kambi kwa kidato cha nne mwaka 2021 zilijadiliwa walienda mbali zaidi na kusema pia kidato cha pili na wenyewe wawekwe kwenye kambi ili kupata muda mzuri wa kujiandaa na mtihani wa Taifa wa kidato cha pili.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.