Wananchi wa wilaya ya Mafia wameaswa kuwa na utaratibu wa kwenda katika vituo vya kutolea huduma ya afya mara kwa mara kwa ajili ya kuchunguza afya zao pamoja na kupatiwa matibabu kabla matatizo hayajawa makubwa.
Wito huo umetolewa leo Juni 14, 2025 na madaktari bingwa waliopo chini ya mpango maalum wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao walioweka kambi katika Hospitali ya Wilaya kuanzia Juni 9, hadi 13, 2025.
" Ni muhimu sana wananchi wawe na tabia ya kufika hospitali mara nyingi maana wanapoendelea kukaa nyumbani, matatizo ya afya waliyonayo yanaweza kuwa makubwa zaidi na kuleta shida kwenye matibabu" ameeleza Grace Matasha, Daktari bingwa wa meno.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wananchi kufika hospitali pindi huduma ya madaktari bingwa inavyowafikia pamoja na kutoa hamasa kwa wengine.
Aidha, ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma ya afya kupitia mpango wake maalum wa kuhakikisha huduma bora inawafikia watanzania wengi katika maeneo yao kupitia madaktari bingwa.
Pamoja na mambo mengi , wananchi wa Mafia wametakiwa kuhakikisha afya za watoto zinaimarika kwa kuzingatia upatikanaji wa lishe bora kama vile ulaji wa mboga kwa wingi ili kuzuia maradhi yanayoweza kujitokeza, ikiwemo selimundu ( sickle cell).
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.