Wajumbe kutoka Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Pwani leo Januari 14, 2025 wamefanya kikao Chao katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Aziza Mangosongo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia, amewapongeza wajumbe kwa kusimamia kwa mafanikio makubwa uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa uliofanyika mwezi Novemba, 2024.
Akiisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mangosongo amewaasa wajumbe kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kwa kutatua kero za wananchi na si kuwa sehemu ya migogoro.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Pwani, Mhe. Zuberi Kizwezwe, amewapongeza wajumbe kutoka halmashauri zote tisa kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kuwataka viongozi kuendelea kutekeleza vyema majukumu yao pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.