Kikao kiliongozwa na mwenyekiti Mhe. Mkuu wa Wilaya Mhandisi Martin Ntemo.
Kikao kilikuwa kwa ajili ya kupokea kero mbalimbali kutoka kwa wajumbe hao.
Kero zilizowalishwa ni pamoja na :-
i.Soko la Kilindoni halina hadhi ya solo la Wilaya na miundombinu yake hairidhishi. Majibu yalitolewa kuwa tayari bajeti ya kutengeneza soko ilishapatikana kupitia mradi wa TASAF.
ii. Postikodi. Baadhi ya watu kukosa namba za nyumba na pia majina ya barabara na mitaa kuwa tofauti na maeneo husika. Akifafanua hoja hii Kaimu mratibu wa zoezi la anwani za makazi na postikodi alieleza kuwa kwa kuwa zoezi la uhakiki limeanza, changamoto zitarekebishwa wakati wa zoezi.
iii. ujenzi wa stendi. Eneo lililopendekezwa ni mtaa wa Shahadadi, kwa kuwa ni eneo la wazi halihitaji fidia . Stendi itajengwa kupitia Mradi wa TASAF
iv. Mlengwa wa TASAF kukosa fedha
maeneo ya miradi yasiyo na fidia kupangiwa miradi yako kwenye mipango miji
v. Migogoro ya mipaka kijiji cha Dongo-kuna tatizo la wenyeviti wa vijiji
kutokujua mipaka yao ambapo idara ya ardhi waliahidi kufufua mipaka iliyopo kwenye gn kwa kuanzia na yenye migogoro na kuwapitia
vi. Mauzo ya viwanja kuuzwa na wanasheria bila kuhusisha majirani wala viongozi kijijini. Akitoa majibu Afisa ardhi alisema
maeneo ambayo yalishapimwa wenyeviti wa vijiji/vitongoji wasishughulike nayo sababu yana nguvu za kisheria
Pia sheria na. 4 ya ardhi inawapa mamlaka viongozi wa vijiji kushiriki katika uuzaji wa maeneo yao na wakati wa kujaza mikataba ya ardhi pia aliwaasa waache kuidhinisha mauziano ya maeneo mara mbilimbili.
Alisema elimu juu ya usimamizi wa sheria ya ardhi itaendelea kutolewa.
Kuhusu kiwanja cha Dawe ndege; mipango miji wana mpango wa kulifanya eneo la michezo, pia kuna chanzo cha maji, changamoto iliyopo ni maji kujaa kipindi cha mvua.
Kuhusu hati - alisema tayari hati zinaendelea kutolewa kwa wahusika na ambazo bado wanaendelea kulishughulikia.
Upimaji wa viwanja vipya. Alisema upimaji unategemea bajeti ya fedha za Halmashauri na Kamishna, pindi fedha ikipatikana zoezi la upimaji litaendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri aliwaasa viongozi kutunza na kuhifadhi mazingira kwani ukataji wa miti hovyo utasababisha jangwa na kuongeza hewa ya ukaa.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.