Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani (KKKT DMP) limeongoza kikao cha tathmini ya mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia ikiwa ni hatua ya kufunga mradi huo uliodumu kwa miaka minne.
Kikao hicho kilichohusisha Halmashauri kupitia Idara za Maendeleo ya Jamii, Afya na Elimu pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Maendeleo lililo chini ya BAKWATA (BAKAID) kimefanyika Julai 16, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia umetekelezwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 kwa ufadhili wa Shirika la Msaada la Norway (NCA) katika kata nne za Ndagoni, Baleni, Chunguruma na Kirongwe ambapo umegusia masuala tofauti yakiwemo utawala bora, kukuza uchumi, msaada wa kisheria, shughuli za ujasiriamali kama ufugaji wa kuku na kilomo cha mboga mboga.
Shirika la Msaada la Norway ( NCA) linatarajia kuwezesha mradi mwingine utakaotekelezwa kwa miaka mitano na Shirika la Maendeleo lililo chini ya BAKWATA (BAKAID).
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.