Wananchi wa Mafia wamejitokeza katika kliniki ya ardhi iliyoandaliwa na Kamishna Msaidizi Mkoa wa Pwani kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amefungua rasmi kliniki hiyo ya siku tatu, leo Juni 18, 2025 ambapo huduma mbalimbali zimetolewa ikiwemo kugawa hatimiliki , kusikiliza kero zihusuzo ardhi, kutoa elimu ya masuala ya ardhi kama vile umuhimu wa kupanga mpango wa ardhi, pamoja na kugawa Ankara za kodi za ardhi.
Kliniki hiyo itafanyika kwa siku tatu ambapo inatarajiwa kukamilika Juni 20, 2025.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.