Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya sheria leo tarehe 3 Februari, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya mihimili mitatu yaani, Bunge, Mahakama na Serikali ili kuhakikisha kuwa haki inapatikana na sheria inazingatiwa
Mhe. Mangosongo ameeleza umuhimu wa ushiriki mzuri wa mabaraza ya kata na wadau mbalimbali ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
" Kuna haja kubwa kwa mabaraza ya kata kupata elimu, nashauri mwaka unaofuata siku kama hii ( maadhimisho ya kilele cha wiki ya sheria) inabidi wajumbe wa mabaraza hayo washiriki " ameeleza Mhe. Mangosongo akitilia mkazo taarifa ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mafia Mhe. Lazaro Magai kuhusu kuhakikisha kwamba shughuli za mahakama zinaakisi Dira ya Maendeleo 2050.
Aidha, ameelezea umuhimu wa haki ya faragha kwa kila mwananchi, hasa kipindi hiki ambacho kuna uhalifu mwingi katika mitandao, akisisitiza kuwepo kwa utoaji wa elimu ya kutosha ili kuepukana na masuala hayo ya uhalifu.
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2025 yameongozwa na kauli mbiu isemayo " Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.