Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Ndugu Mussa Kitungi amekabidhi pikipiki mbili kwa maafisa afya wa kata ya Kilindoni na Kanga, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya, maji na usafi wa mazingira.
Pikipiki hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa SWASH unaotekelezwa kwa njia ya EP4R ( Lipa kulingana na matokeo), ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ilipokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 447 kutoka Serikali Kuu ambazo zimetumika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi Mtendaji ametambua mchango wa mdau THPS kwa hatua hiyo pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri mabilioni ya fedha ambazo zimetumika kuboresha huduma kwa wananchi wa Mafia.
Aidha, amewasisitiza maafisa afya kutunza na kuzitumia kwa lengo la kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wao, maafisa afya wameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kumhakikishia Mkurugenzi Mtendaji kuwa watatunza na kutumia pikipiki hizo kwa malengo lililokusudiwa.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.