Maafisa Waandikishaji ngazi ya kata wametakiwa kutoa hamasa katika maeneo yao ili wananchi waweze kushiriki ipasavyo katika zoezi la uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Hayo yamesemwa leo Februari 7, 2025 na Afisa Mwandikishaji wa Wilaya Ndg. Mohammed Hussein alivyokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kata akiwasisitiza kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wananchi wenye sifa wanajitokeza na kupata haki yao ya msingi ya kikatiba ili waweze kuchagua viongozi wao.
Mafunzo hayo yaliyoanza Februari 6, 2025 yamelenga kutoa uelewa na ujuzi maalum kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ili waweze kutekeleza kwa nadharia na vitendo yale yote yaliyofundishwa.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kuanza Februari 13 na kukamilika ifikapo Februari 19, 2025.
" Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.