Naibu Waziri wa Maji Mhe. Maryprisca Mahundi amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mafia upatikanaji wa maji safi na salama kupitia miradi inayotekelezwa wilayani humo.
Mhe. Mahundi ameyasema hayo alipokuwa akitembelea miradi ya maji iliyomo wilayani Mafia katika kata ya Jibondo, Kilindoni na Kirongwe katika kijiji cha Jimbo kitongoji cha Kidika.
Tuna dhamira kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa kuyaleta maji bombani. Tunakupongeza Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa mahusiano yako mazuri na ofisi yetu ya RUWASA hapa wilayani ambayo yamekuwa chachu ya miradi kukamilika" alisema Naibu waziri Mhe. Mhandisi Mahundi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe.Zephania Sumaye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Mafia kwa kushirikiana na Wiizara ya Maji.
Utekelezaji wa miradi ya maji una lengo la kufikisha maji Safi na salama katika maeneo yote nchini ambapo kwa mijini, huduma ya maji safi na salama inatakiwa kufika asilimia 95 na zaidi hadi kufika mwaka 2025.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.