Halmashairi ya Wilaya ya Mafia inatarajia kupokea watumishi wapya wa sekta ya elimu kufuatia ahadi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa wakati wa ziara yake wilayani Mafia Desemba 13, 2025.
Akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Mwawani ambapo ujenzi wa shule mpya ya msingi unaendelea, Mhe. Kwagilwa ameeleza kuwa kati ya ajira 12,000 zinazotarajiwa kutolewa na Serikali nchini, wilaya ya Mafia itanufaika kwa kiasi kikubwa ili kutatua tatizo la uhaba wa walimu.


" Tunatarajia kutoa ajira 12,000 za walimu nchini, zoezi hili litafanyika kwa awamu ambapo miongoni mwa ajira 7000 katika awamu ya kwanza, Mafia itanufaika kwa kupangiwa walimu ili kutatua changamoto ya uhaba wa walimu" alieleza. Mhe. Rais ameleta fedha nyingi kujenga shule ili kusaidia wanafunzi kutosafiri umbali mrefu, hivyo hatuwezi kuacha miundombinu hii ibaki bila walimu" aliongeza.
Katika hatua nyingine ya kutatua changamoto katika sekta ya Elimu, Mhe. Kwagilwa ameitaka TARURA wilayani Mafia kuharakisha mchakato wa ujenzi wa barabara ya KM 5 itakayorahisisha ufikaji shuleni hapo na maeneo mengine ya Kitongoji.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.