Shirika la ActionAid Tanzania kupitia ActionAid Mafia LRP na Global Platform Tanzania wakiambatana na ofisi ya mkuu wa wilaya Mafia wameendesha zoezi la utoaji elimu ya mpiga kura kwa makundi ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupiga kura kwa usahihi.
Zoezi hili lililofanyika Oktoba 23, 2025 kwa ushirikiano na ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mafia, limejumuisha wanufaika kutoka kata zote nane za wilaya ya Mafia.


Aidha kupitia kampeni hiyo, ActionAid Tanzania wametoa wito kwa makundi hayo pamoja na jamii kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba kwa kuchagua viongozi wao watakaochangia kuleta maendeleo katika Taifa.
" Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura "


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.