Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndg. Mussa Kitungi, akiwa na Timu ya Wataalam ya Halmashauri (CMT), viongozi wa Taasisi zikiwemo TANESCO, RUWASA na TARURA, amefanya ziara ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za mradi wa shule mpya ya Msingi katika kitongoji cha Mwawani, kijlichopo kijiji cha Kifinge kata ya Baleni Novemba 22, 2024.
Ndugu Kitungi amewataka wananchi wa kitongoji hicho kushirikiana vyema na Halmashauri li kukamilisha mradi huo ambao unatarajiwa kuwasaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata masomo yao.
Hatua za awali za maandalizi ya utekelezaji wa mradi zimefanyika ambapo wananchi wameshiriki kusafisha eneo la mradi, hata hivyo hatua kubwa bado zinahitajika ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa maji, umeme na usafi zaidi wa eneo ili kukamilisha mradi kwa wakati.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.