Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ( CMT) leo Aprili 23, 2025 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa wilayani.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mwalo uliopo kijiji cha Chunguruma, ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Jimbo, ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mwawani, zahanati ya Kibada, ujenzi wa shule ya amali kijiji cha Dongo, eneo la machinjio kata ya Kilindoni, utengenezaji wa madawati, viti na meza kwa ajili ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari, ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Kilimahewa na ujenzi wa soko la Halmashauri lililopo kata ya Kilindoni.
Menejimenti imewataka wasimamizi katika maeneo ya miradi kuhakikisha wanaongeza kasi ya utekelezaji pamoja na kuzingatia ubora wa miradi hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
|
|
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.