Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alipotembelea banda la maonesho ya viwanda na biashara Pwani siku ya leo 07.10.2022 amesema kuwa PAPAPOTWE ni lazima atangazwe ndani na nje ya nchi hasa huko DIASPORA ili watanzania wenzetu waliopo huko watuletee watalii wengi kisiwani Mafia.
Amesema ili kufikia lengo la makusanyo la halmashauri kupitia utalii hasa huyu samaki mkubwa ajulikanaye kwa jina la papapotwe ( Whaleshark)Kwa Wingi yapaswa atangazwe kimataifa zaidi
kunakotokana na mapato ya ushuru wa Samaki Mkubwa Bahari ya Hindi Samaki Papa Potwe yapaswa atangzwe kimataifa kwa watalii watakapokuja kwa wingi watachangia pato la wananchi , wilaya na taifa la Tanzania kwa ujumla.
Aliongeza kea kusema kuwa " Utalii ndani ya kisiwa cha Mafia ni sehemu ya chanzo cha mapato kwa jamii na Taifa Wito wangu atunzwe ahifadhiwe na alindwe lengo likiwa kukuza uchumi wa buliu na kuinua hali za Watu wa Mafia na Taifa Kwa ujumla.
Mwisho alimwagiza Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya Mafia Bw. Mohamed Hussein kufuatilia kwa karibu maombi ya boti 10 za kisasa ambazo halmashauri walioomba kwa ajili ya doria, shughuli za Uvuvi na halmashauri zitakazosaidia kuongeza mapato ya halmashauri yatokanayo na mazao ya bahari
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.