Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi ameongoza kikao cha kamati tendaji ya TEHAMA ( ICT STEERING COMMITTEE) kulichojadili utekelezaji wa shughuli za kitengo cha TEHAMA kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Kamati hiyo imejadili juu ya uboreshaji wa huduma kwa jamii kupitia mifumo ya kidijitali ya TEHAMA, usalama wa taarifa za umma, pamoja na kuboresha ufanisi wa kazi za Halmashauri na Serikali kwa ujumla kupitia njia za kidijitali.


Ndugu Kitungi ameitaka kamati hiyo pamoja na Kitengo cha TEHAMA kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwa kushirikiana ili jamii ipate huduma kwa wakati na kwa ubora zaidi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bi. Catherine Tarimo ameieleza kamati juu ya hatua zilizopo za kuboresha mifumo mbalimbali ikiwemo GoTHOMIS katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo wilayani pamoja na mpango uliopo wa kuhakikisha kuwa Halmashauri inahamia katika matumizi ya mfumo wa kidigitali wa kuendesha vikao ( e- Board).
Pamoja na mambo mengine, kamati imepitia sera pamoja na mkakati wa TEHAMA zitakazoongoza Halmashauri katika masuala yote yahusuyo TEHAMA.

Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.