Mnamo tarehe 27/8/2021 , Mkurugenzi Mtendaji (W) Mwl. Kassim S. Ndumbo alifanya kikao na wazabuni , watoa huduma pamoja na wafanyabiashara waliopo Wilayani Mafia ambao ndo wadau wakubwa wa Maendeleo.Aliwaasa kukuza mitaji yao ili kukidhi mahitaji ya tenda wanazopewa, kushirikiana, kuleta bidhaa zenye ubora na viwango elekezi, wasiwe kikwazo Cha kukwamisha miradi kwa kuchelewesha bidhaa agizwa, kuwa matumizi sahihi ya lugha kati ya wauzaji na wanunuzi (zisizokwaza) pia kuwa na wasimamizi wenye utaalamu na wanaojua taratibu za manunuzi ya Umma Kama quotation n.k
Kwa upande wa wafanyabiashara walitoa maoni yao kuwa taarifa ya kikao hicho walichelewa kuipata hivyo kupelekea wadau wengi kushindwa kuhudhuria walimuomba Mkurugenzi aandae tena kikao kama hicho na awape taarifa mapema ili wapate muda wa kujiandaa na kuhudhuria kikao hicho kwa wingi.
Aidha katika kikao hicho alialikwa pia Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mh. Eng. Martin Mtemo na aliwashauri wawe na uongozi wao kwa wakati huu waunde wa mpito ili taarifa ziwafikie kirahisi
Pili ianzishwe redio ya jamii itakayoweza kurahisisha mawasiliano
Tatu, wafanyabiashara biashara waunganishe nguvu ili kuweza kufanya kazi kubwa pindi inapotokea
Nne, wawe na madaftari ya kutunzia kumbukumbu za manunuzi na mauzo pia wakati wa kuchukua zabuni waweke tahadhari (business risk) za usafirishaji wa bidhaa, bima, dharura
Tano, Kuwa na vikao (forum) za wafanyabiashara kwa ajili ya kufundishana na kuelekezana namna za kufanya biashara.
Mwisho aliwaondoa hofu kuwa halmashauri inafunga mikataba inapokuwa na fedha na kwa Sasa Mafia Ina miradi ya takriban bilioni tano ( 05)
Kutoka ofisi ya Mbunge aliwaomba viongozi na wafanyabiashara kumuunga mkono mwakilishi wao bungeni kwa kutumia vizuri na kwa wakati fedha inayoletwa Wilayani .Mwisho walikubaliana tarehe ya kikao kuwa jumatatu ya tarehe 13/09/2021 saa 4:00 asubuhi na wenye agenda za kujadiliwa zifikishwe kwa sekretarieti .
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.