Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Kassim S Ndumbo alifanya kikao na mawakala wa kukusanya ushuru wa Halmashauri siku ya Kumbukumbu ya baba wa Taifa tarehe 14/10/2022.
Katika kikao hicho walihudhuria pia maafisa kutoka kitengo cha Fedha na Uhasibu , Utumishi na utawala, Mipango na uratibu, kitengo cha TEHAMA na Kitengo cha Manunuzi
Katika kikao hicho Mkurugenzi aliwapongeza mawakala na watendaji wote wanaofanya Vizuri katika kukusanya ushuru wa halmashauri kupitia vyanzo mbalimbali kwa kufanikisha kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwani juhudi yao ndiyo iliyofanikisha kufikia lengo na kuvuka
Aliwaasa kuipenda kazi yao kukusanya mapato ya halmashauri na kuifanya kwa uaminifu kwani ndiyo inayowapatia riziki na kusisitiza atakayebainika anafanya njama yoyote ili kukwepa ushuru hatavumiliwa.
Kuweka pesa benki kwa wakati kwa sheria ya fedha inavyotaka na kuondoa hoja za ukaguzi na pia matumizi ya fedha mbichi.
Ikitokea wakala amepata dharura yoyote itakayomfanya ashindwe kukusanya ushuru basi atoe taarifa ofisi ya mwekahazina kwani mashine ikionekana haifanyi kazi (offline) zinaleta hoja za ukaguzi
Aliendelea kusema pia fedha ya mapato ya ndani wanayokusanya 40% inarudi kufanya miradi ya maendeleo ambapo tayari machinjio , soko la samaki kilindoni yamefanyiwa ukarabati mkubwa, madawati yametengenezwa na kusambazwa shuleni, na mradi tarajiwa wa kutengeneza daraja la kwa msomanga tayari fedha zimetengwa.
Aidha Afisa TEHAMA (W) aliwaasa kuwa waangalifu na kufanya kazi kwa umakini mkubwa kuepuka kukosea muamala na kukagua rola kabla ya kutoa risiti na kama ikitokea bahati mbaya umekosea kukata muamala aidha kuzidisha pesa ama hitilafu yoyote katika mashine itakayosababisha muamala kusoma pesa kubwa ama risiti kutoka mara mbili watoe taarifa na wafuate taratibu wa kufuta muamala huo kabla ya kuweka benki fedha ili kuepuka usumbufu wa kushindwa kuweka pesa kwa wakati
Kwa upande wa mawakala walisema wanamshukuru Mkurugenzi Mtendaji (W) kwa kuona umuhimu wa kuwakutanisha pia walitoa mapendekezo ya vyanzo vipya ambavyo bado havikusanywi vikiwemo mafuta ya nazi na vyuma chakavu
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.