• Wasiliana nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mafia District Council
Mafia District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi, Mipango miji na Maliasili
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
        • Kitengo cha Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi na Zima Mmoto
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango na Takwimu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Tehama
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Huduma za jamii
      • Maadili
      • Fedha, Utawala, na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Kujua Sheria
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
      • YOUTUBE
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUTANO WA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA UHIFADHI WA BAHARI NA MAENEO TENGEFU

Posted on: July 4th, 2024

Ili bahari iweze kutupatia manufaa, kuna umuhimu mkubwa wa kutunza vitu vilivyomo ndani yake vikiwemo nyasi bahari, matumbawe na mikoko ili viweze kutupatia rasilimali hai.

Kwa kuzingatia umuhimu huo,Taasisi ya  Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), The University of Queensland na Coral Reef Rescue Initiative, wameandaa Mradi wa Kuokoa Matumbawe unaolenga kujenga taasisi, mifumo na miundombinu ya kuweza kusimamia na kuokoa matumbawe.

Akizungumza wakati wa mkutano wa ushirikishwaji wa wananchi na ngazi mbalimbali za Serikali Wilayani Mafia, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amemshukuru Mhe.  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele sekt…

Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele sekta ya mazingira nchini pamoja na kutoa wito kwa mashirika binafsi kujikita katika utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake, Mratibu wa Uhifadhi katika Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Uhifadhi wa Matumbawe, Ndugu Godfrey Ngupula, ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano mzuri ili kuweza kufikia lengo la mradi.

" Kuanzia viongozi wa juu, wataalam, wanasheria, Halmashauri, wafanyabiashara na wananchi wote kwa pamoja tuweze kuzungumzia hali ya matumbawe na kuhakikisha tunayahifadhi; kwa kuzingatia ripoti zetu Mpango Mkakati wa Kitaifa tulionao tunaenda kuona nini kifanyike kama jamii ili tuhakikishe rasilimali zinatufaa" alisema Ndugu Ngupula.

Wavuvi, wachakataji samaki  pamoja na wakulima wa mwani wamepongeza kuwepo kwa mradi huo wilayani na kuweka nia ya kushirikiana na Serikali katika kutunza mazingira, hasa matumbawe ili kuendelea kunufaika na rasilimali za baharini.

" Tunaishukuru Serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuhifadhi mazingira na kutuwezesha wavuvi na wakulima wa mwani kufanya shughuli zetu, elimu hii itatusaidia kufanya kazi zetu kwa ufanisi mkubwa" alisema Issa Kombo, mvuvi na mchakataji wa samaki.

" Natoa wito kwa wavuvi wenzangu kupokea elimu hii na kuifanyia kazi, wenzetu wanatuletea mradi ambao ni wa muda mfupi lakini uvuvi ni endelevu, hivyo sisi tuna jukumu kubwa kutekeleza tuliyojifunza" aliongeza Kombo.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Mazingira Duniani ( GEF) utatekelezwa kwa miaka minne katika nchi saba ikiwemo Tanzania; nchi nyingine ni Madagascar,  Indonesia, Philippines, Salomon Islands, Fiji na Cuba, ambapo katika awamu ya kwanza ya mradi, nchi sita zitaanza utekelezaji ikiwemo Tanzania.

Zaidi ya asilimia 25 ya aina za samaki duniani zinapatikana kwenye matumbawe huku zaidi ya asilimia 70 ya uvuvi mdogo nchini Tanzania unafanyika kwenye matumbawe, hivyo ni muhimu kuyatunza ili kunusuru uvuvi na shughuli nyingine baharini zikiwemo ukulima wa mwani na utalii kwa manufaa ya jamii na Taifa kiujumla.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KULIPIA VIWANJA May 20, 2025
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • WITO WATOLEWA KWA WATOTO WA KIKE KUPENDA MASOMO YA SAYANSI

    May 17, 2025
  • MAFIA KUUNGANISHWA NA UMEME WA GRIDI YA TAIFA

    May 16, 2025
  • WANANCHI WAASWA KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LARIDHIA KUANZISHWA KWA MRADI WA UONGEZAJI THAMANI ZAO LA DAGAA

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

MWENGE WA UHURU WAPONGEZA VIWANGO VYA BARABARA YA MSUFINI
Tazama Video zaidi

Viungo vya haraka

  • Home
  • Photo Gallery
  • FAQ
  • Tourism
  • Investment
  • MATOKEO YA STD VII 2022

Viungo vinavyohusiana

  • OR- TAMISEMI
  • OR- Menejimenti Utumishi wa Umma
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Wizara ya Fedha na Mipango

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kilindoni-Bomani Street

    Anuani ya posta: 85

    Simu: 0232010199

    Simu ya mkononi:

    Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Katazo
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma namba 1
    • YOUTUBE

Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.