Taasisi isiyokuwa ya kiserikali iitwayo Relevant Company Ltd ya Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Mafia wamefanya kikao kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira na biashara ya hewa ya ukaa. Washiriki wa kikao walikua ni wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri, waheshimiwa madiwani, Taasisi za Marine park, Action aid, WWF ,TFS na wajumbe kutoka ofisi mbunge, mwenyekiti wa CCM wilaya. Kikao hicho kililenga jamii kuhifadhi misitu kwa ajili ya kupunguza hewa ya ukaa na ruzuku itatolewa kwa misitu ya serikali na watu binafsi endapo wataridhia kukubali mradi huo ambao unatatajiwa kufadhiliwa na Shirika la Carbon market lililoko nchini Marekani. Washiriki waliridhia na kuomba iandaliwe hati ya maridhiano baada ya wananchi kuridhia pia.