Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Maendeleo ( UNCDF) pamoja na Kampuni ya OIKOS, imetembelea wilaya ya Mafia kwa lengo la kuhakiki maeneo yaliyobainishwa kuathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa wilayani Mafia, wamepata fursa ya kufanya majadiliano na Timu ya Utekelezaji wa Mradi ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Mussa Kitungi, pamoja na kutembelea eneo la Bondeni Pwani ambapo mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unatarajiwa kutekelezwa.
Mradi huo unatarajiwa kuboresha mazingira na maisha ya wananchi, hasa wanaojihusisha na shughuli za uvuvi pamoja na utalii ambao wamekuwa wakiathiriwa na mabadiliko ya tabianchi hasa katika eneo hilo ambalo limekuwa likiharibiwa na maji mara kwa mara.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.