Mradi wa Shule Bora Tanzania umetoa mafunzo kwa maafisa elimu kata, walimu wakuu pamoja na walimu wa hisabati wa shule za msingi zilizopo wilayani.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Februari 20, 2025, Mratibu wa Programu ya Shule Bora mkoa wa Pwani Ndg. Ng'wigulu Kube ameeleza kuwa wao ni watu wa muhimu katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya elimu na Serikali inawategemea, hivyo waongeze umakini katika utendaji kazi kwakuwa Serikali inawajengea uwezo ili wafikie malengo.
Mradi wa Shule Bora ni mradi wa Serikali unaofadhiliwa na UKAID kwa lengo la kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuboresha Elimu.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuendelea tena hapo kesho kwa washiriki , ambapo walimu wa hisabati watajifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kufundisha somo hilo kwa vitendo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.