Mradi wa Shule Bora leo 25 Februari, 2025 umeendelea kutoa mafunzo kwa kuwawezesha Maafisa Elimu Kata, Walimu Wakuu na Walimu juu ya mbinu mbalimbali za usimamizi na ufundishaji.
Katika mafunzo hayo, Maafisa Elimu na Walimu Wakuu wamejifunza kuhusu usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji pamoja na uundaji wa MEWAKA na Jumuiya za Kujifunza kwa madarasa ya kwanza na pili.
Mafunzo kwa walimu yalihusu mbinu za ufundishaji na stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ( KKK) kwa kuzingatia mtaala ulioboreshwa, aidha wamejifunza jinsi ya kutengeneza zana za kujifunzia na kujifundishia
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.