Mradi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya #Mafia umefikia asilimia 45 ya utekelezaji wake. Mradi huu unagharimu jumla ya Shilingi Milioni 520 ambapo kati ya fedha hizo, Milioni 270 zimetolewa na wadau wa kuimarisha huduma za uzazi na afya ya mtoto KOFIH, na Milioni 250 zimetoka serikali kuu.
Mradi unatarajiwa kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi, kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto pamoja na kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya Mafia.
Hivi karibuni hospitali ilipokea vifaa tiba vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa Tanzania @msd ikiwa ni muendelezo wa kuboresha utoaji wa huduma za #afya wilayani.
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia inatoa shukrani kwa serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe. Rais Dkt. @samia kwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huu ili kutatua changamoto za huduma za #afya.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.