Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Ndugu Mussa Abdul Kitungi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Ndugu Kitungi ameyasema hayo leo Septemba 26, 2024 alipokuwa akitoa taarifa kwa Umma kuhusu maelekezo ya uchaguzi.
Amesisitiza kuwa, wananchi wanayo haki na wajibu wa kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024 na kwba kwa mujibu wa kanuni ya 31 ( GN571), uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na wajumbe wa halmashauri ya kijiji, utafanyika kwenye kitongoji na vituo vingine vilivyoelekezwa katika vijiji husika.
Aidha, ametoa wito kwa wakazi wenye sifa za kugombea nafasi ya mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na wajumbe wa halmashauri ya kijiji, kuchukua fomu za kugombea kutoka katika ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
Kwa upande wao, viongozi wa vyama vya kisiasa wilayani wamepongeza hatua hiyo na kuiomba Serikali kuhakikisha kuwa inasimamia haki na amani ili kufanikisha upatikanaji wa viongozi bora.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.