Matukio mbalimbali yakimuonesha Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Petro Magoti wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba kata ya Kiegeani ambapo vijana 18 wamehitimu mafunzo yao yaliyoanza Aprili 14, 2025.
Mhe. Magoti ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwashika mkono vijana kupitia programu mbalimbali za kitaifa ambapo vijana hao wanatarajiwa kupata ajira ya kudumu na kuanza kazi ifikapo Septemba mosi mwaka huu 2025
Aidha, amewapongeza kwa kujitoa kulitumikia taifa lao na kuwataka kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya rushwa.
Mhe. Magoti alipata fursa ya kutembelea miradi ya afya ( jengo la mama na mtoto) katika Hospitali ya Wilaya, pamoja na soko la Kilindoni ambapo amewapongeza wasimamizi wa miradi kwa kutekeleza vizuri maagizo ambayo yataleta mchango mkubwa katika kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.