Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Aziza Mangosongo amepokea Timu ya Wataalam kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Timu hiyo iliyoongozwa na Dkt. Siafu Sempeo, imefika wilayani Mafia Novemba 08, 2024 kwa ajili ya kufanya tathmini ya programu ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Shule ( IPOSA), ambayo Serikali inatarajia kuanzisha wilayani mwanzoni mwa mwaka 2025.
Miongoni mwa malengo ya mpango huo wa IPOSA ni pamoja na, kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), kujenga stadi za Ujasiriamali kwa vijana, stadi za maisha na sadi za ufundi wa awali ambapo programu inawalenga zaidi vijana wenye umri wa miaka 14 au zaidi, vijana waliodondoka shule za msingi, vijana waliohitimu shule za MEMKWA, na mabinti wadogo walioacha shule kwa sababu ya ujauzito.
Programu hii inatekelezwa nchini katika mikoa tofauti ikiwemo mkoa wa Pwani, ambapo kwa Wilaya ya Mafia, mpango utatekelezwa kwa kujenga jengo maalum la karakana ( Workshop) kwa ajili ya kufundishia Stadi za Maisha ( Ufundi Stadi) katika shule ya msingi Kilindoni.
Miongoni mwa fani zitakazotolewa ni pamoja na Ushonaji, Useremala na Uashi.
Mpango huo ulioanzishwa mwaka 2019, unatekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na wafadhili mbalimbali likiwemo Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea ( KOICA).
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.