Serikali imelenga kuongeza ajira kwa vijana kupitia vyuo vya VETA kwa kuongeza uzalishaji na usindikaji bora wa mazao yanayozalishwa nchini ikiwa ni njia bora ya kuongeza mnyororo wa thamani.
Hayo yamesemwa leo Agosti 07, 2024 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Mafia Mh. Omar Kipanga alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya nanenane mkoani Morogoro alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Mhe. Kipanga amesisitiza umuhimu wa mafunzo kuhusu dhana ya uchumi wa buluu katika kukuza uchumi kisiwani Mafia na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametumia fursa ya maonesho hayo kuwakaribisha wawekezaji wilayani Mafia ili waweze kuleta mchango wao katika kuinua uchumi.
"Mungu ametubariki watu wa Pwani kwa kuwa na mambo ya kipekee, tunaweza kujipatia manufaa makubwa kutokana na Uchumi wa Buluu, maana sisi ukanda wetu huu tumezungukwa na bahari" alisema Mhe. Mangosongo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.