Ikiwa ni siku ya pili ya maonesho ya Tamasha la Utalii ( Mafia Island Festival) viongozi kutoka taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za serikali, wafanyabiashara, wadau wa utalii pamoja na wananchi kwa ujumla wamejitokeza kushiriki Tamasha hilo kwa kutembelea mabanda ya maonesho.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo ambaye ni mgeni rasmi kwa siku ya leo Desemba 7, 2024 ameelezea umuhimu wa kuboresha miundombinu wilayani Mafia, hasa usafiri wa anga na maji.
"Mafia sasa inaendelea kufunguka, hivyo watalii wanaoingia ni wengi, jukumu letu la msingi lililopo ni kuhakikisha panafikika kwa urahisi" alisema Kanali Kolombo akielezea hali ya usafiri kisiwani ambapo ametoa wito kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuboresha kiwanja cha ndege kwakuwa hivi sasa safari za ndege haziwezi kufanyika usiku, kwakuwa hakuna taa zinazowezesha ndege kutua usiku.
Aidha, ameelezea umuhimu wa kuboresha usafiri wa majini ili kupunguza changamoto kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Asha Salim ameipongeza Wilaya ya Mafia kwa kuandaa Tamasha huku akielezea mchango wake katika kukuza utalii na utamaduni kisiwani Mafia na Taifa kwa ujumla.
" Matamasha kama haya ni muhimu sana katika kuendeleza, kuibua, kukuza utamaduni wetu wa manzanita ikiwemo sanaa" alisema Dkt. Asha
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Kanali Kolombo walipata fursa ya kushuhudia mashindano ya michezo mbalimbali na kutembelea mabanda ya maonesho kuona bidhaa na huduma zitolewazo na wadau wa utalii, uhifadhi mazingira na wafanyabiashara kwa ujumla, hasa katika masuala ya uchumi wa buluu.
Tamasha hilo linatarajiwa kumalizika ifikapo kesho Desemba 8, 2024.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.