Sheikh wa Wilaya ya Mafia, Nuhu Abubakar Swalihu, akikakabidhi futari kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ikiwa ni zawadi kutoka kwa Sheikh wa Mkoa wa Pwani, Abasi Mtupa.
Akipokea zawadi hizo, Mhe. Mangosongo ametoa shukrani kwa Sheikh wa Mkoa na kuelekeza zawadi hizo kusaidia wanafunzi wa bweni wa shule ya sekondari ya Jibondo katika kipindi hiki cha Ramadhani.
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na mchele kilo 250, maharage kilo 100, unga wa sembe kilo 10, mafuta ya kula lita 20, sukari kilo 40, tambi katoni mbili na boksi moja ya tende.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.