Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametoa wito kwa jamii kuwa kila mwananchi kwa nafasi yake, awajibike kutunza mazingira ili Serikali na kila mmoja aweze kunufaika.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Papa Potwe Duniani yaliyofanyika leo Agosti 30, 2025 Mhe. Mangosongo amesisiitiza umuhimu wa kutunza mazingira ikiwa ni njia kubwa ya kuhakikisha kuwa rasilimali za bahari zinakuwa salama ili ziweze kunufaisha wananchi kiuchumi hasa wanaojihusisha na shughuli za utalii na uvuvi.
Aidha, ameitaka Halmashauri kusimamia vizuri sheria ndogo zinazohusu utunzaji wa mazingira ili viongozi mbalimbali katika ngazi za kata na vijiji pamoja na taasisi zisizo za kiserikali ziweze kuwajibika ipasavyo kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.