Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanasimamia vyema malezi ya watoto ili kujenga jamii yenye maadili mazuri.
Mhe. Mangosongo ameyasema hayo leo Februari 11, 2025 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Msufini kilichopo kata ya Kilindoni, akigusia matukio mbalimbali ambayo tamekuwa yakikithiri ikiwemo utoro kwa wanafunzi, ukatili wa kijinsia pamoja na wizi.
Ameeleza kwamba miongoni mwa maeneo yenye shida kwa upande wa maadili ni kitongoji cha Msufini ambapo matukio mbalimbali yamekuwa yakiripotiwa ambayo mengi yamesababisha watoto kutofika shuleni na kujihusisha na vitendo vya kihalifu.
Aidha, amewataka wazazi kuwajibika kwa kushirikiana na serikali ya kijiji na viongozi mbalimbali wilayani ili kufichua vitendo viovu ambavyo vinachangia kuharibu jamii.
Tabia ya utoro shuleni imepelekea wanafunzi kujihusisha na shughuli za uvuvi ambayo baadhi ya wazazi wamekuwa wakiilalamikia, huku wakiiomba Serikali iwasaidie kufuatilia wamiliki na waongozaji wa yombo vyote vya uvuvi ambao wanatoa ajira kwa watoto.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.