Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Aziza Mangosongo amewaongoza wakazi wa wilaya ya Mafia katika tamasha la uchaguzi lililofanyika Oktoba 10, 2024 likilenga kutoa hamasa kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Mafia na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga, Katibu Tawala Bw. Shaban Shabani, kamati ya usalama, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mussa Kitungi na Wakuu wa Idara na Vitengo, Mhe. Mangosongo alitumia tamasha hilo kutoa wito kwa wakazi wote wenye sifa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa ifikapo Oktoba 11, 2024 ili waweze kushiriki uchaguzi ifikapo Novemba 27, 2024.
Zoezi la kujiandikisha litadumu kwa siku kumi, hadi ifikapo Oktoba 20, 2024.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.