Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikitoa mrejesho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Bw Musa Kitungi baada ya kukamilisha ziara ya usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma za Afya ya Msingi vilivyopo wilayani Mafia.
Zoezi hilo limelenga kufanya ufuatiliaji wa ukamilishaji wa miundombinu ya Afya (kama majengo), utoaji wa huduma za Afya, ustawi wa jamii na lishe, pamoja na uwepo wa dawa na vifaa tiba.


Katika ziara hiyo timu imepitia na kukagua uwekezaji mkubwa uliofanyika na Serikali ikiwemo ujenzi wa Majengo ya huduma za Dharura (EMD), Majengo ya wagonjwa mahututi (ICU), jengo la huduma za Uzazi (maternity Complex) na mtambo wa uzlishaji hewa Tiba (oxygen Plant).
Timu ya usimamizi shirikishi imepokea taarifa na mipango ya Wilaya ya Mafia katika kuimarisha huduma za Afya ukiakisi uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali iiwemo mapokezi makubwa ya vifaa na vifaa tiba. Aidha timu imepokea maombi ya Hospitali ya Mafia ya fedha za ukarabati wa hospitali ya Wilaya Ili kuboresha zaidi utolewaji wa huduma hasa ikizingatiwa upekee na jiografia ya Wilaya ya Mafia.
Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru Serikali Kwa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo kutoa fedha za kujikimu, uhamisho na likizo na kuahidi kuendelea kusimamia maslahi hayo hasa yaliopo katika mamlaka ya Wilaya.

Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.