Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia umepongezwa kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa hosteli ya wasichana katika shule ya Sekondari ya Kilindoni unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF).
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Shadrack Mziray alipokuwa ameambatana na timu yake katika ziara kukagua mradi huo ambao umefikia hatua za mwisho za utekelezaji.
Mziray ametoa rai kwa uongozi wa Halmashauri kuongeza nguvu zaidi ili mradi ukamilike kwa wakati na katika ubora unaotarajiwa ili wanafunzi waweze kunufaika.
Mradi huo uliofikia asilimia 77 ya utekelezaji, unatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 220 mpaka utakapokamilika na kuanza kutumika.
Katika utekelezaji wa mradi , jamii imeshiriki kwa kutoa nguvu kazi kama utoaji wa visiki, kumwagilia kuta za jengo, kutengeneza vitanda kwa ajili ya wanafunzi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.