Mkuu wa wilaya Mafia Mh.Aziza Mangosongo amepokea magodoro 100 yenye thamani ya shilingi laki tano kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kwa lengo la kuwasaidia wafungwa wa magereza ya Kilindoni na magereza ya Kilombero.
Akipokea Magodoro hayo leo Desemba 17, 2025, Mhe. Mangosongo ameishukuru TFS kwa msaada huo na kuwataka viongozi katika magereza hayo kuhakikisha kuwa yanatunzwa na kutumika kwa kazi iliyokusudiwa.


Akikabidhi Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi Prf.Dos Santos Silayo,Kamanda wa Kanda ya Mashariki Methu Ntilicha ameelezea kuwa lengo la kukabidhi magodoro hayo ni kuchangia juhudi za kimaendeleo kisiwani hapo.Kwa upande wake, Mrakibu mwandamizi wa magereza wilaya ya Mafia Ndugu Gastory Suline ameahidi kuhakikisha kwamba magodoro waliyokabidhiwa yanatunzwa na kutumika kama ilivyokusudiwa.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.