Bodi ya Watalii Tanzania ( TTB) imeipongeza Wilaya ya Mafia kwa kujitoa kwa dhati kuhakikisha kwamba mradi wa ujenzi wa kituo cha michezo unafanikishwa na kutekelezwa kwa kutenga eneo maalum la mradi huo.
Hayo yamewekwa wazi na Mwenyekiti wa Bodi ya Watalii, Dkt. Ramadhan Dau wakati wa ziara ya Bodi hiyo walipotembelea kijiji cha Gonge katika kata ya Baleni.
Ziara hiyo imelenga kutafuta fursa za uwekezaji , kujifunza na kutambua vivutio vya utalii pamoja na kukutana na wawekezaji waliopo kisiwani Mafia.
"Kwa nia thabiti ambayo mmeionesha, imetupa sisi nguvu kwamba kweli mradi huu ukija Mafia tutapata ushirikiano mkubwa na hakutakuwa na matatizo yoyote" alisema Dkt. Dau.
Kwa upande wake, Mkurugenzi w Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Ephraim Mafuru amesema "kwa sababu sisi ni Bodi inayohusika na kutangaza, ni muhimu sana tukahamasisha namna bora ya kutangaza utalii wa Mafia". Mafia ni kisiwa ambacho ni cha pekee duniani" aliongeza
Hayo yamejiri wakati ambapo wilaya ya Mafia inajindaa na Tamasha la Utalii lijulikanalo kama " Mafia Island Festival " linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 6 na kumalizika tarehe 8 Desemba, 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametumia fursa hiyo kuiomba TTB kuisaidia kuitangaza Mafia mara kwa mara kupitia vipindi vya Televisheni na Redio ili wananchi na Dunia nzima kutambua mazuri yaliyopo Mafia ikiwemo vivutio vya utalii na fursa nyingi za uwekezaji.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.