Tume ya Madini Tanzania imefanya ziara yake wilayani Mafia kwa lengo la kukagua na kutambua maeneo ambayo shughuli za uchimbaji wa madini ujenzi zinafanyika.
Tume hiyo imesisitiza wachimbaji kufuata sheria na taratibu ikiwemo kuwa na leseni pamoja na kibali kutoka mamlaka husika ndani ya Halmashauri huku ikidhamiria kupanga bei elekezi ya madini ujenzi ambayo hapo awali haikupangwa wilayani Mafia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ameiagiza Halmashauri kupitia Idara ya ardhi kuhakikisha kwamba inatenga maeneo maalum ya uchimbaji pamoja na kuzingatia utunzaji wa mazingira na kuwaelekeza wasafirishaji wa madini hayo kuwajibika kwa kushirikiana na TARURA na uongozi wa vijiji katika kukarabati barabara.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.