Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ameitaka Halmashauri kuongeza mapato kwa kuweka mipango thabiti ya kubuni vyanzo vipya pamoja na kusimamia vizuri vyanzo vilivyopo.
Mhe. Mangosongo ameyasema hayo leo Novemba 14, 2024 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliojadili taarifa za utekelezaji wa Shughuli za kamati za kudumu kwa kipindi cha robo ya kwanza, 2024.
Amewataka viongozi wa Halmashauri wakiwemo Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha Halmashauri haipotezi mapato yake.
" Niwaombe sana Wakuu wa Idara na Vitengo na Wananchi tushirikiane kwa pamoja kuongeza mapato, kulipa kodi ni takwa la nchi na la dini pia" alisema Mhe. Mangosongo.
Aidha, ametumia mkutano huo kuendelea kuwasisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kujitokeza kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 27 Novemba, 2024 kwa kuhakikisha kuwa kila aliyejiandikisha anakwenda kupiga kura.
Miongoni mwa mambo mengine, ametumia pia fursa kuwaalika wananchi wote katika Tamasha la Utalii linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 06 hadi 08 Disemba, 2024 lijulikanalo kama " Mafia Island Festival ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.