Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ameshiriki mchezo wa bao la kete pamoja na wananchi wa kata ya Kilindoni katika mashindano aliyoandaa kwa lengo la kudumisha utamaduni, upendo pamoja na mahusiano mazuri katika jamii.
Mashindano hayo yamedumu kwa siku mbili kuanzia Julai 12 hadi 13, 2025 na kuhusisha washiriki 40 waliounda timu 10 kutoka maeneo mbalimbali ya kata ya Kilindoni huku wakishindania nafasi tatu.
Mhe. Mangosongo amewashukuru washiriki wote kwa kujitokeza na kuwa tayari kuenzi tamaduni na kuhakikisha wanadumisha upendo, umoja na amani katika jamii pamoja na kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha masuala ya michezo na utamaduni yanapatiwa kipaumbele.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla katika masuala ya michezo na kuahidi kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu na hatua itakayofuata ni kuandaa mashindano hayo katika kata ya Kirongwe na baadaye kuendesha mashindano kiwilaya.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.