Wakazi wa wilaya ya Mafia wameendelea kutoa kutoa hamasa kuelekea Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa kwa kushiriki mazoezi pamoja na usafi wa pamoja.
Katika kudumisha taratibu za usafi wa mazingira, watumishi wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mussa Kitungi, viongozi wa vyombo vya usalama na taasisi mbalimbali, vikundi vya hamasa vya michezo na wananchi kwa ujumla, wameshiriki mbio za polepole na kufanya usafi maeneo mbalimbali katika kata ya Kilindoni.
Hayo yamejiri wakati zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa likianza rasmi leo Oktoba 26 na kudumu hadi ifikapo Novemba 01, 2024.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi ".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.