Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kuweka mazingira mazuri kwa kuteleleza miradi mbalimbali itakayosaidia kukuza uwekezaji nchini
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara pamoja na uzalishaji wa umeme wa uhakika utakaokidhi mahitaji ya wawekezaji nchini.
Hayo yamewekwa wazi na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega wakati akifunga wiki ya maonesho ya Biashara na Uwekezaji ya mkoa wa Pwani leo Desemba 20, 2024 katika viwanja vya Maili Moja.
Waziri Ulega ameeleza kuwa ili kupandisha hadhi mji wa Kibaha, Serikali imetenga Shilingi Bilioni moja itakayotumika kutanua barabara ya kutoka Maili Moja hadi Picha ya ndege hatua ambayo itasaidia kuondoa adha ya foleni na kutatua kero kwa wawekezaji.
Aidha, amepongeza kazi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Taifa linakua kiuwekezaji ambapo kwa mara ya kwanza katika Taifa, kwa mwaka 2024 kumekuwa na uingiaji mkubwa wa mitaji kutoka nje; jumla ya Dola za kimarekani Bilioni 42.1 zimeingia nchini kwa ajili ya masuala ya uwekezaji.
Maonesho ya Biashara na Uwekezaji ya Mkoa wa Pwani yaliyohitimishwa leo, yamedumu kwa siku tano tangu Desemba 16 2024.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.