Wananchi wilayani Mafia, leo Oktoba 5, 2024 wameungana na Uongozi wa Halmashauri, viongozi wa vyama vya siasa, watumishi, vikundi vya michezo ( jogging) pamoja na vikundi vingine katika jamii katika mbio za polepole ikiwa ni lengo la kufanya mazoezi na kutoa hamasa kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kufuatia hatua hiyo, msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Ndugu Mussa Kitungi amewapongeza wakazi wa Mafia, watumishi na vikundi vyote vya hamasa kujitokeza kushiriki mazoezi pamoja na kutoa hamasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika Novemba 27 mwaka huu.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kugombea nafasi za uongozi pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ifikapo Oktoba 11 hadi 20, 2024.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.