Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amezindua rasmi ugawaji wa vyandarua Oktoba 7, 2025 katika zahanati ya Kilindoni ambapo jumla ya vyandarua 50,937 vinatarajiwa kugawiwa kwa kaya 23, 311.
Hii ni mwendelezo wa hatua nyingi ambazo Serikali inaendelea kuchukua kutokomeza malaria hasa katika wiilaya ya Mafia ambayo ni miongoni mwa halmashauri za mkoa wa Pwani zenye maambukizi ya juu ya Malaria.


Hata hivyo, kiwango cha maambukizi ya Malaria kimepungua kutoka asilimia 12% mwaka 2024 hadi kufikia 11.3% kwa mwezi Agosti, 2025 ambapo idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na Malaria imepungua kwa asilimia 1.3% kutoka wagonjwa 4646 mwaka 2024 hadi wagonjwa 2592 mwezi Agosti 2025.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.