Timu ya Wataalam ya Halmashauri (CMT), ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Mussa Kitungi, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa wilayani hususan miradi ya elimu na afya Oktoba 09, 2024.
Akiwa ziarani, Ndugu Kitungi amewataka wasimamizi wa miradi kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi waweze kupata huduma kwa wakati, pamoja na ushirikishwaji wa wananchi.
Aidha, amewapongeza viongozi na wananchi wa kitongoji cha Mwawani kilichopo kijiji cha Kifinge, kata ya Baleni kwa kuwa mfano mzuri kwa kuonesha ushirikiano na mshikamano katika masuala ya maendeleo, hasa katika maandalizi ya mradi wa shule mpya ya msingi inayotarajiwa kujengwa.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya msingi Bweni, eneo linalotarajiwa kujengwa shule ya sekondari Jimbo, shule ya msingi Sharaza, eneo linalotarajiwa kujengwa shule ya msingi Mwawani, shule ya msingi Sikula, eneo linalotarajiwa kujengwa shule ya sekondari ya amali lililopo Dongo na jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.