Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Zephania Sumaye amewahakikishia wakazi wa Mafia kwamba serikali imepunguza ushuru wa bandarini ambapo hapo awali ulikuwa ukitozwa mara mbili kwa bandari za Nyamisati iliyopo Kibiti pamoja na bandari ya Mafia.
Mhe. Sumaye ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi, uliofanyika katika kitongoji cha Msufini kilichopo kata ya Kilindoni tarehe 9 Septemba 2023.
Hapo awali usafiri wa majini ulileta changamoto kwa wananchi, hasa wafanya biashara kwa kutozwa ushuru mara mbili kwa bandari za Nyamisati na Mafia.
Kufuatia punguzo hilo la tozo, Mhe. Sumaye alitumia fursa hiyo kuwasihi wafanya biashara waliopo Mafia kupunguza bei za bidhaa zao.
"Tunataka tuone matokeo ya kupunguzwa kwa ushuru huo kwa wananchi wa kawaida, maana ni malengo ya serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanayostahili kwa bei inayostahili" alisema Mhe. Sumaye.
Mafanikio haya ni matunda ya ushirikiano mzuri kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia na Mamlaka ya Bandari Tanzania kuhakikisha wananchi wanapata nafuu ya ushuru katika usafiri na bei za bidhaa.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.