Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Pwani, umefanya ziara ya kutembelea waathirika wa Maafa ya Kimbunga " Hidaya" wilayani Mafia Mei 29, 2024.
Ziara hiyo imelenga kutoa pole kwa waathirika wote wilayani pamoja na kutoa misaada kwa waengwa.
Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Bi. Zaynab Matitu Vulu amepongeza juhudi za Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa ajili ya wakazi wa Mafia.
" Tumeona tuje Mafia ambapo maafa yalikuwa makubwa sana, tunawapa pole na kumshukuru Mhe. Rais Samia kwa msaada alioutanguliza hapa, wadau mbalimbali pamoja na mbunge wa Mafia, Mhe. Omar Kipanga" alisema Bi. Matitu.
Misaada iliyokabidhiwa ni pamoja na mabati na misumari, kamba kwa ajili ya wakulima wa mwani, nguo za wakubwa na watoto na miswaki.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametoa shukran zake za dhati kwa UWT na kutoa wito kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya kisiwa cha Mafia kujitokeza kusaidia waathirika wa maafa.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.