Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Aziza Mangosongo, leo Aprili 23, 2024 amezindua chanjo ya Kansa ya Mlango wa Kizazi (HPV) kwa wasichana wa umri kuanzia miaka 9 hadi 14 kiwilaya katika Shule ya Sekondari Kitomondo.
Mhe. Mangosongo ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zinazotolewa kwa wakati.
"Takwimu zinaonesha Tanzania, kwa nchi za Afrika Mashariki tunaongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya wa saratani, hii inasababishwa na wanawake wengi kuchelewa kufika katika vituo vya kutolea huduma. Hivyo ni vyema kama msichana, ama mtoto wa umri huo kupata chanjo" alisema Mhe. Mangosongo.
Mhe. Mangosongo ameipongeza Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo kwa kuendelea na kampeni ya kuzuia magonjwa ya saratani pamoja na magonjwa mengine kama surua.
Watoto 4826 wilayani Mafia wanatarajiwa kupata chanjo ya Kansa ya Mlango wa Kizazi ( HPV) kati ya watoto 147648 wa mkoa wa Pwani.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.